Posts

Showing posts from June, 2019

AINA YA BIASHARA UNAWEZA ANZISHA PASIPO KUWA NA HELA (mtaji-fedha)/kidogo Sana.

Image
Wengi huamini kuwa lazima uwe na fedha ndio uanzishe biashara na ndio sababu yao kuu ya kukaa bila kujishughulisha,Ukweli ni kwamba mtaji ni moja ya kitu muhimu sana katika kuanzisha biashara,lakini kuna aina ya biashara ambazo zinahitaji gharama ndogo sana kuanzisha na kukupelekea kupata faida kubwa sana.Kama mfanyabiashara unaweza kutoka kwa kishindo sana  kwa kuanza ukiwa huna kitu na kufanya kazi kwa juhudi sana ukiwa upande wa huduma(services) na kufanikiwa kutengeneza faida kubwa na kutokea hapo na kuanza kufikiria kuanza kukodi ofisi yako,kuajiri watu wengine nk ,ingawa ni rahisi kutoka ukiwa upande wa huduma lakini inahitaji ujuzi au weledi Fulani hivi ili uweze fika kilele cha mafanikio hapa simaanishi lazima uwe umesoma chuo kikuu maana ujuzi au utaalamu wa jambo halihusiani na degree ya chuo kikuu. Unaweza pata ujuzi kwa kuhudhuria semina mbalimbali,workshop mbalimbali,au kufundishwa na mtu wenye ujuzi husika na baada ya kupata ujuzi kuanza fanyia kazi kati...

AINA MBILI ZA MAWAZO.

Image
➕MTU MWENYE MAWAZO CHANYA. ➖MTU MWENYE MAWAZO HASI. ---------------------- ➕Mtu mwenye mawazo chanya, siku zote huwa ni mwenye Ratiba na mipango. ➖Mtu mwenye mawazo hasi, siku zote huwa ni mwenye visingizio. . ➕Mtu mwenye mawazo chanya, siku zote yeye mwenyewe ni sehemu ya majibu. ➖Mtu mwenye mawazo hasi, daima ni mtu mwenye kulalamikia matatizo. ➕Mtu mwenye mawazo chanya, katika kila jambo gumu huiona fursa. ➖Mtu mwenye mawazo hasi, katika kila fursa kwake ni jambo gumu. ➕Mtu mwenye mawazo chanya, hutafuta njia ya utatuzi wa matatizo. ➖Mtu mwenye mawazo hasi, huiona njia ya utatuzi kuwa ndio tatizo. ➕Mtu mwenye mawazo chanya, daima huzidisha marafiki. ➖Mtu mwenye mawazo hasi, siku zote huzidisha maadui. ➕Mtu mwenye mawazo chanya, siku zote hutenda jambo linalokubalika na wengi. ➖Mtu mwenye mawazo hasi, hukata tamaa ya kufanya jambo  linalokubalika na wengi. ➕Mtu mwenye mawazo chanya, siku zote hutatua matatizo kwa kuvuta subira. ➖Mtu mw...

KWANINI TUNACHELEWA KUYAFIKIA MAFANIKIO YETU KWA HARAKA?? PATR 1.

Image
----------------------------------- KATIKA SAFARI YANGU YA KUTAFUTA SABABU, NILIJARIBU KUTAFAKARI MAANA YA NENO COMPANY (YAANI KAMPUNI), COMPANY NI NENO LA KIINGEREZA LENYE MAAA YA USHIRIKA. UHIRIKA KATIKA HISA NA BIASHARA NA MAUZO NA HATA MAPATO. MOJAWAPO YA SABABU ZA KUCHELEWA KUFIKIA MAFANIKIO YETU NI UBANIFASI WA KUTEGEMEA MAWAZO YETU BILA KUSHIRIKISHA MAWAZO YA WENGINE (KWA MAANA YA USHIRIKA). JIFUNZE KUMJENGEA MWENZAKO DHANA NZURI, HAKIKA USHIRIKA WENU UTALETA MAFANIKIO YA HARAKA. ----------------------------------- DAIMA KUMBUKA KUWA UJASIRIAMALI SIO KAZI! UJASIRIAMALI NI MFUMO WA MAISHA . NA: JB KAZINGATI