AINA MBILI ZA MAWAZO.





➕MTU MWENYE MAWAZO CHANYA.
➖MTU MWENYE MAWAZO HASI.
----------------------

➕Mtu mwenye mawazo chanya, siku zote huwa ni mwenye Ratiba na mipango.
➖Mtu mwenye mawazo hasi, siku zote huwa ni mwenye visingizio.
.
➕Mtu mwenye mawazo chanya, siku zote yeye mwenyewe ni sehemu ya majibu.
➖Mtu mwenye mawazo hasi, daima ni mtu mwenye kulalamikia matatizo.

➕Mtu mwenye mawazo chanya, katika kila jambo gumu huiona fursa.
➖Mtu mwenye mawazo hasi, katika kila fursa kwake ni jambo gumu.

➕Mtu mwenye mawazo chanya, hutafuta njia ya utatuzi wa matatizo.
➖Mtu mwenye mawazo hasi, huiona njia ya utatuzi kuwa ndio tatizo.

➕Mtu mwenye mawazo chanya, daima huzidisha marafiki.
➖Mtu mwenye mawazo hasi, siku zote huzidisha maadui.

➕Mtu mwenye mawazo chanya, siku zote hutenda jambo linalokubalika na wengi.
➖Mtu mwenye mawazo hasi, hukata tamaa ya kufanya jambo  linalokubalika na wengi.

➕Mtu mwenye mawazo chanya, siku zote hutatua matatizo kwa kuvuta subira.
➖Mtu mwenye mawazo hasi, daima huzidisha matatizo kwa hasira zake.
----------------------

(Jitahidi kuwa mtu mwenye mawazo chanya)
💡💡💡💡💡💡
www.kazingati.blogspot.com
Jb Kazingati.
💡💡💡💡💡💡

Comments

Popular posts from this blog

SIRI 31 ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA

MANENO KUNTU... JISOMEE MWENYEWE.

MAMBO 7 MUHIMU KWA MWENYE NDOTO YA KUWA MFANYABIASHARA MKUBWA.